MFUKO WA MAFAO YA KUSTAAFU
RETIREMENT BENEFITS FUND
Menu

Jikwamue Scheme "Boda Boda Scheme"

NANI ANAWEZA KUJIUNGA NA JIKWAMUE SCHEME?

Wadau wote waliojiajiri katika sekta ya usafirishaji Kwa njia ya boda boda na bajaji ambao ni madereva, vikundi na wamiliki wa Boda boda/ Bajaji.
 

FAIDA YA KUJIUNGA NA JIKWAMUE SCHEME

 • Kuwakinga madereva boda boda dhidi ya majanga kwa kuwapa mafao kutoka GEPF
 • Kuwawezesha dereva boda boda kupata mikopo ya riba nafuu kwa ajili ya kukuza biashara zao kama kununua piki piki n.k
 • Kuwajengea dereva boda boda utamaduni wa kujiwekea akiba ili kuweza kutimiza malengo yao ya baadae.
   

JINSI YA KUJIUNGA

 • Ili Kujiunga na Jikwamue scheme fika katika moja ya ofisi za GEPF, utajiunga na kupatiwa kitambulisho cha uanachama hapo hapo. 
 • Hakuna gharama yoyote ya kujiunga na Mfuko wa GEPF.
   

JINSI YA KUCHANGIA

 • Hakuna kima cha chini cha uchangiaji mwanachama anaruhusiwa kujichangia kiasi chochote
 • Mwanachama anaweza kuchangia kwa njia ya Simu (M-Pesa, Tigo Pesa au Airtel Money), Benki, Mawakala Waliothibitishwa na GEPF au Kuwasilisha moja kwa moja kwenye ofisi za Mfuko wa GEPF.
   

MIKOPO KWA WANACHAMA WA JIKWAMUE SCHEME

 • Wanachama wa jikwamue Scheme watapata fursa ya kupata mikopo kutoka GEPF kwa njia ya mtu mmoja mmoja au kupitia vikundi kwa ajili ya kuendeleza biashara zao.
 • Kiasi cha Mkopo huu kitategemea akiba aliyojiwekea Mwanachama katika mfuko wa GEPF au jumla ya akiba za wanachama wa kikundi.
 • Mikopo hii inaanzia kiasi cha Tsh 250,000.
 • Mwanachama anatakiwa awe amechangia kwa muda wa miezi 6 tu ili kupata mkopo huu.

 

Download Application Form