MFUKO WA MAFAO YA KUSTAAFU
RETIREMENT BENEFITS FUND
Menu

Mkopo wa Kuanza Maisha: “Daka Mkwanja na GEPF”

Nani Anapaswa Kupatiwa Mkopo Huu?

Ni mwanachama yoyote aliejiunga na Mfuko kutoka katika sekta ya umma, Serikali Kuu na Serikali za Mtaa ambao ndio ajira zao za kwanza.

Mkopo huu maalumu ni kusaidia waajiriwa wapya hivyo hauna sharti la muda wa kuchangia isipokua mwanachama lazima awe ameripoti katika kituo cha kazi na kuoikea angalau mshahara wa mwezi mmoja.

 

Masharti ya kupata mkopo

v  Awe ameajiriwa katika sekta ya Umma

v  Kiwango cha juu cha mkopo huu ni mishahara ya miezi 2

v  Mwanachama atarejesha mkopo huu kupitia makato ya mshahara kwa kipindi cha miaka 2.

 

Faida za Mkopo huu

v  Mwanachama atapatiwa mkopo huu mara tu baada ya kuajiriwa bila kujali muda aliochangia katika mfuko.

v  Mkopo wenye riba nafuu zaidi katika soko la fedha.

v  Kumuwezesha mwanachama kumudu gharama za awali anapoanza ajira mfano kodi ya nyumba, fenicha n.k.

v  Makato madogo katika mshahara wa mwanachama kwa kulinganisha na muda wa marejesho. 
 

Download Application Form